Tume ya TEHAMA,VETA sasa kushirikiana katika vyuo saba

DAR-Tume ya TEHAMA inaendelea kupanua wigo wa kukuza ubunifu na kuendeleza sekta ya TEHAMA nchini, baada ya kuingia makubaliano na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ya kuendeleza teknolojia katika vyuo saba vya VETA vya wilaya kwa kipindi cha miaka mitano.
Makubaliano hayo yamefikiwa kwa kusaini mikataba ya ushirikiano, kila upande ukisaini mikataba hiyo kupitia Wakurugenzi wake wakuu, Dkt. Nkundwe Mwasaga wa Tume ya TEHAMA na CPA Anthony Kasore wa VETA.

Akizungumza wakati wa tukio huko, Dkt. Mwasaga amesema; kazi ya tume yake katika mkataba huo itakuwa ni pamoja na kuweka vifaa vya TEHAMA katika karakana za vyuo hivyo.
Amefafanua kuwa, inawajibika kufanya hilo na mengine, kwa kuwa moja ya majukumu ya Tume yake ni kuendeleza TEHAMA ambapo vijana ndio fursa yao kuingia na kuonesha ubunifu kupitia sekta ya TEHAMA.

Naye CPA Kasore alisema Tume ya TEHAMA itasaidia katika kuongeza ujuzi katika masuala ya Teknolojia kwenye vyuo vya VETA.
Aliongeza kuwa, suala la Teknolojia linakuwa kila siku hivyo ni fursa ya vijana kupata ujuzi wa teknolojia ya TEHAMA kabla ya kuingia katika soko la ajira.

Amevitaja vyuo saba vitavyonufaika na makubaliano ya mafunzo ya TEHAMA ni katika Wilaya za Mpanda, Singida, Njombe, Morogoro, Songea, Mpanda pamoja na Singida.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news