Wananchi waonesha utayari Mradi wa Medeli Phase III

DODOMA-Wananchi wa Dodoma na mikoa jirani wameonesha utayari wa kuchangamkia nyumba za mradi mpya wa Medeli Awamu ya Tatu (Medeli Phase III) ambao unatekelezwa na Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) jijini Dodoma.
Mradi huo ambao unatajwa kuwa wa aina yake, maafisa masoko na biashara wa NHC wamewaeleza wananchi kuwa,si tu utakuwa na majengo ya kisasa.

Pia,utakuwa na mandhari ya kuvutia, maegesho ya kutosha, usalama wa uhakika na mahali pazuri pa kuishi au kuwekeza.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na maafisa hao kupitia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi kwa Umma ambayo yalianza Juni 16,2025 na kufikia tamati leo Juni 23,2025 katika viwanja vya Chinangali Park jijini hapa.

Aidha,maadhimisho hayo yalifunguliwa Juni 17,2025 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mheshimiwa George Simbachawene huku leo yakifungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amezindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa, ujulikanao kama Government Enterprises Service Bus (GovESB).

Sambamba na Mfumo wa pili ni wa e-Wekeza unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida Fund).
Siku ya Utumishi wa Umma husherehekewa kila Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news