UCSAF yatoa elimu kwa Machifu na Sekretarieti ya AWADEF

DODOMA-Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umetoa elimu kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa Machifu wa Mikoa ya Kusini na Sekretarieti ya Akida Wabu Development Foundation (AWADEF).
Mafunzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya UCSAF jijini Dodoma, kwa lengo kuwaelimisha viongozi hao wa jadi na wawakilishi wa asasi juu ya majukumu na fursa zinazotolewa na UCSAF katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika maeneo ya pembezoni na yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Mafunzo hayo yalilenga pia kuimarisha ushirikiano kati ya UCSAF na wadau wa maendeleo ya jamii ili kuhakikisha jamii mbalimbali nchini, zinapata elimu kuhusu huduma za mawasiliano zinazowezeshwa na Serikali kupitia UCSAF katika maeneo yao.

Akielezea kuhusu mafunzo hayo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Bw. Kitandu Ugula alisema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Mfuko katika kujenga uelewa mpana kwa wadau mbalimbali kuhusu vipaumbele vyake, hususan katika kufikisha huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini.

Machifu na wawakilishi wa AWADEF, walitoa pongezi kwa UCSAF na kuahidi kushirikiana kwa karibu katika kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news