ARUSHA-Idara ya Uhamiaji imesema imemzuia Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Godbless Lema kutoka nchini na kuishikilia pasipoti yake katika kituo cha uhamiaji cha mpaka wa Namanga mkoani Arusha, pamoja na kumtaka kuripoti katika ofisi za Uhamiaji kwa ajili ya mahojiano.
Idara imesema kuzuiwa kwa Lema ni utaratibu wa kawaida unaotumika kwa raia yeyote pale ambapo idara imepata taarifa zinazohitaji mhusika kuhojiwa.
Aidha, imetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa zilizotolewa na Lema kupitia mitandao ya kijamii kuwa zuio hilo linawalenga viongozi wa CHADEMA.

