Wakali wa mabao Ligi Kuu ya NBC

KIUNGO wa Simba, Jean Ahoua ameendeleza ubabe akihusika katika mabao mengi zaidi kuliko wachezaji wengine wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025 hadi sasa.
Ahoua ambaye amejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu amefanikiwa kufunga mabao 15 na kutoa pasi za mabao nane hivyo kuhusika katika mabao 23.

Prince Dube wa Young Africans anashika nafasi ya pili baada ya kuhusika katika mabao 21 akifanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani mara 13 na kutoa pasi za mabao nane ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya timu hiyo akitokea Azam FC.

Pacome Zouzoua wa Young Africans nae hajabaki nyuma akiwa amefanikiwa kuhusika katika mabao 18 baada ya kufunga mabao 9 na kutoa pasi za mabao 9.

Kwa upande wake Feisal Salum wa timu ya Azam amehusika katika mabao 17 akiwa ametoa pasi za mabao 13 na kufunga mabao 6 huku akiwa kinara wa kutoa pasi za mabao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news