Wanahabari wakongwe Tanzania waonesha upendo wa agape kwa Rais Dkt.Samia kama walivyofanya wabunge

DODOMA-Wakati wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimuenzi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumtunuku TUZO MAALUM,waandishi wa vitabu vinavyoelezea mafanikio ya Dkt. Samia wamekutana na kubadilishana vitabu vyao katika kuonesha ushirikiano katika kazi yao.
Waandishi hawa wakongwe,Gaston Modest Kaziri wa taasisi ya DEVCOM ambaye ameandika kitabu cha The Sixth phase Government of Dr. Samia Suluhu Hassan Presidency, "We are delivering" (kushoto) na Derek K. Murusuri aliyeandika kitabu cha Samia na Falsafa ya Samialojia (kitabu cha 4R) (kulia), wakibadilishana vitabu vyao wakionesha mfano kwa waandishi wengine chipukizi.

"Sisi si washindani bali ni washirika tunaoandaa maudhui yanayoi-brand Tanzania na uongozi wake wa juu, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha maendeleo ya taifa la Tanzania," walisema.

Waandishi hawa wa habari waandamizi ambao wamevutiwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wameandika vitabu vitakavyosomwa na vizazi vijavyo, vikijifunza na kuhamasishwa na mchango wa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuiletea maendeleo Tanzania.

Bw. Kaziri ambaye pia ni mwanafunzi wa digrii ya uzamivu, PhD, aliwahi kufanya kazi ya uandishi wa habari katika vyombo mbalimbali vya habari nchini, vikiwamo Uhuru na Mzalendo na Guardian.

Naye Bw. Murusuri, alipata kuwa afisa habari msaidizi katika Idara ya Habari (MAELEZO) na pia akafanya kazi kama Mwandishi wa Habari wa Katibu Mkuu wa CCM na Msaidizi wa Waziri wa Nchi (Mipango).

Falsafa ya 4R ya Dkt. Samia ni muarobaini wa migogoro ya kisiasa barani Afrika na imeiwezesha Tanzania kuwa nchi ya mfano katika ujenzi wa utamaduni wa maridhiano, ambao umesaidia kuleta amani nchini.

"Haya yote yametugusa, kila mmoja kwa wakati wake, kuamua kuyaandika katika vitabu ili vizazi vijavyo vifahamu mchango adhim wa kiongozi wetu katika safari ya maendeleo ya taifa letu," alisema Bw. Kaziri.
Bw. Kaziri pia amebobea katika tafiti za mapinduzi ya viwanda nchini na katika ukanda wa SADC.

Bw. Murusuri alisema, falsafa ya 4R imeiheshimisha sana Tanzania kwa vile Dkt. Samia anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka Afrika, katika kizazi hiki, ambaye anatoa suluhisho la migogoro ya dunia kupitia falsafa yake ya 4R.

Matokeo ya Salsafa hii ya 4R ambayo Bw.Murusuri ameiita SAMIALOJIA, imesaidia kuleta mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii ndani ya muda mfupi. Walio na macho wameshuhudia. Amani imetamalaki. Maendeleo yamepatikana.

Jana Mei 31, 2025 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilimtunuku TUZO MAALUM Dkt. Samia kwa kutambua uongozi wake katika kipindi cha miaka minne.

"Kipindi cha miaka minne cha uongozi wako kiliakisi utawala bora, weledi, uwajibikaji, uaminifu na ujumuishi," alisema Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt.Tulia Ackson.
"Kwa nafasi yetu Wabunge, tumeshuhudia historia ya mafanikio na mabadiliko [mageuzi] yaliyoleta tija na ustawi kwa jamii nzima," alisema.

Dkt. Tulia aliongeza kuwa, "tunapokusanyika hapa, tunaadhimisha na kuutambua mchango wako kupitia tuzo hii maalum."

Kesho Juni 2, 2025 vitabu hivyo viwili vitapatikana katika viwanja vya Bunge la Tanzania jijini Dodoma, katika maonesho ya siku tano hadi Ijumaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news