DAR-Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanakopa katika maeneo rasmi ili kuondoa changamoto ya mikopo umiza ambayo imekuwa ikileta adha kwa wananchi kwa kufilisiwa mali zao.
Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo amesema Serikali imeweka utaratibu wa kujisajili kwa watoa huduma za fedha ili kukomesha tatizo hilo.
Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu, ambapo Wizara ya Fedha na taasisi zake zinashiriki kikamilifu kutoa huduma kwa karibu kwa wananchi kupitia Maonesho hayo.




