DODOMA-Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo, na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Nsajigwa Kabigi, wametembelea banda la Tume ya Madini katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayohitimishwa leo katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, viongozi hao wamejionea namna Tume ya Madini inavyoshiriki kikamilifu katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake, huduma mbalimbali zinazotolewa na mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa rasilimali za madini nchini.Mhandisi Lwamo sambamba na kuwapongeza wataalam waliopo kwenye banda hilo, amewataka kuendelea kutoa huduma kwa weledi, uwazi na ubunifu kwa kuzingatia mabadiliko ya kidijitali ili kuwawezesha wananchi kupata taarifa kwa haraka na kwa usahihi.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni: “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”, ambayo inalenga kuimarisha utendaji katika utumishi wa umma kupitia matumizi ya teknolojia.





