DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ((Mb) ameungana na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kumuaga Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili nchini, ambapo alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Bara la Afrika ikiwemo Tanzania kupitia uongozi wake
Pia,baadae aliungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutembelea na kukagua miradi miwili ya kimkakati inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ukiwemo ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa kilomita 112.3, katika eneo la Mtumba, jijini Dodoma.Sambamba na Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma, unaohusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na miundombinu mingine.








