DAR-Katibu Mkuu wa Bakwata, Alhaj Nuhu Jabir Mruma amethibitisha kuwa, katika Baraza la Eid El Adha litakalofanyia kesho Jumamosi Juni 7,2025 baada ya Sala ya Eid, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Alhaj Jabir Mruma amewaomba Waislam kuhudhuria katika Sala ya Eid mapema kesho katika Msikiti wa Mfalme Muhammad Sadia IV Bakwata makao makuu Kinondoni, Dar Es salaam.
