Naibu Katibu Mkuu Mwandumbya ateta na ujumbe wa Kampuni ya ALSTOM

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya ALSTOM yenye makao yake makuu nchini Ufaransa, iliyoonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi na uendeshaji wa miundombinu ya reli ili kupunguza msongamano wa magari na kuboresha usafiri katika jiji la Dar es Salaam.
Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini, Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) Wizara ya Fedha, Bw. Bashiru Taratibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), Bw. David Kafulila, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Kampuni ya ALSTOM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news