MKOA wa Iringa unajiandaa kupokea wanamichezo kutoka mikoa mbalimbali nchini, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Tanzania kwa shule za Msingi na Sekondari yanayotarajia kuanza tarehe 7 Juni 2025.
Mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwaka yanaratibiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita tangu 2022, mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA yalifanyika Mkoani Tabora, na mwaka huu yanafanyika Mkoani Iringa yakitarajiwa kuhusisha wanamichezo zaidi ya 7,000 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
