MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji ambaye pia anaziwakilisha Madagascar na Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na Mhe. Antoine Kola Masala Ne Beby, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) nchini Msumbiji kwenye Ofisi za Ubalozi huo jijini Maputo.
Wakati wa mkutano huo wa Julai 3,2025 ambao ni mwendelezo wa mikutano ya Mhe. Balozi Hamad kujitambulisha, waheshimiwa mabalozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa kihistori kati ya Tanzania na DRC kwa maslahi ya pande zote mbili.

