Balozi CP Hamad ateta na Waziri Mkuu wa Msumbiji

MAPUTO-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji,Mheshimiwa CP Hamad Khamis Hamad amekutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe.Maria Benvinda Levy jijini Maputo tarehe 09 Julai, 2025 kwa ajili ya kujitambulisha.
Mazungumzo ya viongozi hao, yalielekeza umuhimu wa kuimarisha biashara ya mipakani na uboreshaji wa miundombinu, hasa kupitia Ukanda wa Maendeleo wa Mtwara,uwekezaji wa pamoja kwa kuzingatia mazingira bora ya sera na sheria yanayochochea sekta binafsi kushiriki kikamilifu.

Mhe. Waziri Mkuu Levy aliahidi kwamba Ofisi yake sambamba na wizara na taasisi nyingine za Serikali ya Msumbiji, zitatoa kila aina ya ushirikiano kwa Mhe. Balozi Hamad ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Naye, Mhe Balozi Hamad alijitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri Mkuu Levy na kueleza shukrani kwa mapokezi mazuri pamoja na ushirikiano mzuri kutoka Serikali ya Msumbiji tangu kuwasili kwake. Pia alisisitiza dhamira ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa karibu kati ya nchi hizi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news