Mama Janeth Magufuli atembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu maonesho ya Sabasaba

DAR-Mke wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Janeth Magufuli ametembelea banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA) Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na viongozi wa ofisi hiyo.
Akiwa katika banda hilo, Mama Janeth alipokelewa na kutembelea kuona namna Ofisi ya Waziri Mkuu inavyohudumia wananchi kupitia idara, vitengo pamoja na taasisi zake.
Aidha, miongoni mwa huduma zinazotolewa na ofisi hiyo ni pamoja na elimu ya masuala ya menejimenti ya maafa, shughuli za Wakala wa Kupigachapa Mkuu wa Serikali, Baraza la Taifa la Biashara, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, elimu ya masuala ya Vyama vya Siasa Nchini, Masuala ya VVU na UKIMWI, Usalama na Afya Mahala Pa Kazi, Masuala ya Watu Wenye Ulemavu, programu ya ASDP II, fursa za vijana pamoja na huduma zinazotolewa na NSSF, PSSSF, WCF na CMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news