NA GODFREY NNKO
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya Bima Na.394 imeanzisha bima ya lazima kwa wageni wanaoingia Tanzania Bara itakayogharimu Dola za Marekani 44.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Julai 4,2025 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Fedha,Bw.Benny Mwaipaja.
Kupitia bima hiyo, mchangiaji atanufaika na huduma za uokoaji, matibabu ya dharura, usaidizi akipoteza mzigo na kurudishwa nyumbani iwapo itatokea dharura.
Aidha,kupitia taarifa hiyo,Bw.Mwaipaja amefafanua kuwa, utekelezaji wake utaanza pale itakapoingizwa katika Gazeti la Serikali na umma utajulishwa;

