TANGA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeshiriki katika uzinduzi wa mradi wa "Focus on Youth, Not Substance", unaolenga kutoa elimu sahihi kwa vijana na jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya na namna ya kujikinga.
Mradi huo umezinduliwa Julai 1, 2025 jijini Tanga ikiwa ni sehemu ya miradi saba chini ya mpango wa Tanga Yetu na unalenga kupambana na matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwa njia ya elimu na uhamasishaji wa tabia chanya, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali Ili kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo vijana, wazazi, wanafunzi na wadau wengine.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)



