MWANZA-Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Ziwa imetoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya na mbinu za kudhibiti matumizi na biashara ya dawa hizo kwa Maafisa, Wakaguzi, na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mwanza.
Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa, lakini pia kukuza ushirikiano wa karibu kati ya taasisi hizo mbili katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa, lakini pia kukuza ushirikiano wa karibu kati ya taasisi hizo mbili katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini.
Akizungumza mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo, Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mwanza (RPO), SACP Kimolo, alimshukuru Kamishna Jenerali Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kuruhusu na kuwezesha utolewaji wa elimu hiyo muhimu kwa watumishi wa Jeshi la Magereza na kueleza kuwa elimu hiyo imekuja wakati muafaka kutokana na mazingira ambayo askari magereza hufanya kazi nayo kila siku.“Askari wetu huishi na wafungwa ambao wanatoka katika mazingira mbalimbali ya kijamii, wakiwa na tabia na hulka tofauti. Baadhi yao wamefungwa kwa makosa ya kuhusika kama matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Kupitia mawasiliano ya karibu baina ya askari na wafungwa, tunapata fursa ya kipekee ya kujifunza kuhusu mwenendo wa biashara hiyo haramu, wakiwemo wahusika na mbinu wanazotumia. Ushirikiano huu na DCEA utatusaidia kuimarisha upashanaji wa taarifa za kiintelijensia,” alisema SACP Kimolo.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Jeshi la Magereza
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)


