DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa njia ya kidijitali ambapo ameongea na Wajumbe wa Mkutano huo Nchi nzima kwa njia ya Mtandao leo tarehe 26, Julai 2025 katika ukumbi wa Mkutano wa NEC (White House) Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.






