Dkt.Natu El-maamry Mwamba afanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania

DAR-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Mhe. Peter Huyghebaert, ambapo wamezungumza kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na nchi hiyo.
Mkutano huo umefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam na  kuhudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedeck Mbise, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubeligiji, Bw. Koenraad Goekint na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano wa Ubeligiji, Bi. Fanny Heylen pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Fedha na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news