Gavana Tutuba azindua rasmi Jarida la Uchumi Wetu toleo Namba 1 la Julai,2025

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amezindua rasmi Jarida la Uchumi Wetu, Toleo Namba 1 la Julai, 2025 linaloandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania kupitia Idara ya Mawasiliano kila baada ya miezi mitatu.
Akizungumza katika uzinduzi wa jarida hilo Gavana Tutuba amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Idara ya Mawasiliano ya Benki Kuu ya Tanzania katika kuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania.
Ameongeza kuwa, Jarida hilo litakuwa ni wenzo wa kuuwezesha umma kusoma habari zihusuzo sekta ya fedha na uchumi wa nchi kiujumla zinazotoka Benki Kuu, Serikalini pamoja na sekta binafsi.
Jarida la Uchumi Wetu limesheheni maarifa kupitia habari, makala na matukio mbalimbali na litasambazwa kwa njia ya nakala tepe (soft copies) kupitia tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania www.bot.go.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news