Waziri Dkt.Nchemba aongoza ujumbe wa Tanzania kikao cha mashauriano ya ndani kuelekea Mkutano wa SCFEA-EAC

ARUSHA-Waziri wa Fedha, Mhe.Dkt.Mwigulu Nchemba ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha mashauriano ya ndani kuelekea katika Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika leo tarehe 25 Julai 2025, Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.
Mkutano huo ambao umehudhuriwa pia na wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwemo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki), Mhe. Dennis Londo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, utajadili pamoja na mambo mengine, hatua za kikodi zilizo kwenye sheria za fedha za nchi wanachama zenye kuleta athari za kubagua bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi za Jumuiya.
Hatua hii ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa 46 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) na makubaliano ya Mawaziri wa Fedha wakati wa mashauriano ya kibajeti katika mikutano yao iliyofanyika mwezi Mei,2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news