DODOMA-Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM Group, Eng. Hersi Said, amesema kuwa maendeleo ya taifa hayawezi kufikiwa bila afya njema ya wananchi na uwekezaji katika jamii.
Ametoa kauli hiyo wakati wa kilele cha NBC Dodoma Marathon 2025, ambapo GSM Group ilishiriki kama mdhamini mkuu kupitia taasisi yake ya kijamii ya GSM Foundation.Katika marathon hiyo, GSM Group imetoa huduma kwa washiriki zaidi ya 12,000 kwa kuwagawia maji safi ya kunywa na vinywaji mbalimbali kutoka GSM Beverages ikiwemo G-Boost, GSM Pop na GSM Cola.
Kupitia GSM Foundation, kampuni imetoa msaada wa kijamii kwa kuunga mkono ajenda za marathon kama vile kuongeza idadi ya wakunga kutoka 100 hadi 200, kupambana na saratani ya mlango wa kizazi na kutoa ufadhili wa masomo kwa wauguzi 100 watakaohudumia watoto wenye changamoto ya usonji (autism).
Kampuni hiyo pia imewatunuku washindi wa mbio za kilomita 10 kwa wanaume na wanawake kwa zawadi mbalimbali zikiwemo vocha za bidhaa za kielektroniki kutoka Haier zenye thamani ya shilingi milioni 4, pamoja na vinywaji, sabuni na tambi kutoka GSM.





