DAR-Kampuni ya iTrust Finance imetangaza rasmi uzinduzi wa Mfuko wa iDollar ambao ni mfuko wa pamoja wa soko la fedha uliobuniwa kwa kutumia Dola ya Marekani (USD).
Uzinduzi huo umeongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),CPA Nicodemus Mkama leo Julai 10,2025 jijini Dar es Salaam.
Mfuko wa iDollar unawafaa watu binafsi na taasisi zinazotafuta uwekezaji ulio salama, katika hati fungani na dhamana za muda mfupi hadi wa kati, huku ukitoa mapato bora zaidi kulingana na amana za kudumu za benki za dollar.
Kwanini Mfuko wa iDollar?
Mfuko huu unalenga kutoa mapato ya ushindani kwa kuwekeza kwenye dhamana zenye mapato ya kudumu za Dollar, ikiwa ni pamoja na amana za muda, na hati fungani za makampuni binafsi.
Aidha,muda wa kuweka bila kutoa ni siku 90 na hakuna ada ya kujitoa katika mfuko wa iDollar ambao utoaji wa fedha ni ndani ya siku tano za kazi.
Pia,wawekezaji wanaopendelea uwekezaji salama na wale wanaotafuta mapato thabiti na yenye utulivu
Wengine ni wawekezaji wenye malengo ya kifedha ya muda mfupi hadi wa kati na wanaotaka kujilinda dhidi ya mabadiliko ya thamani ya Shilingi ya Tanzania
Miongoni mwa faida kwa mwekezaji ni pamoja na kuwa na mapato ya juu kuliko yale ya amana za kudumu za benki za dola ikiwemo urahisi wa kutoa fedha ndani ya siku tano za kazi.
Faida nyingine ni udhibiti chini ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na usalama kupitia Benki ya CRDB Plc ikiwemo mapato bila kodi kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Faida nyingine za kuwekeza iDollar ni kupata usimamizi wa kitaalamu kupitia wachambuzi mahiri.
Kutoka iTrust Finance
"Lengo letu kupitia Mfuko wa iDollar ni kuwawezesha Watanzania kupata jukwaa salama,rahisi, na lenye faida la kukuza akiba zao kwa kutumia Dollar ya Marekani," alisema Msemaji wa iTrust Finance.
"Katika mazingira ya sasa ya mabadiliko ya sarafu yasiyotabirika, tunajivunia kutoa suluhisho lenye uthabiti, uwazi na upatikanaji kwa wote."
Kuhusu iTrust Finance
iTrust Finance Limited ni mtoa huduma za kifedha anayesimamiwa na kupewa leseni na Benki ya Tanzania na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kama mkopeshaji wa Daraja la 2 na Meneja wa Mfuko, Wakala wa Hisa na Mshauri wa Uwekezaji mtawalia.
iTrust Finance Limited ina ofisi yake Masaki, Mtaa wa Mahando 429, Jengo C jijini Dar es Salaam,
Tanzania.
Meneja aliingizwa kama kampuni binafsi tarehe 24 Oktoba 2013 akiwa na Cheti cha kampuni Namba 103309 chini ya Sheria ya Makampuni ya 2002.
iTrust Finance Limited katika kazi zake za Masoko ya Mitaji (Uwakala wa Hisa, Usimamizi wa mifuko, na Ushauri wa Uwekezaji) inasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana.