Jonathan Sowah wa Singida Black Stars ajiunga na Simba SC

SINGIDA-Klabu ya Singida Black Stars imethibitisha kuwa mshambuliaji wao Jonathan Sowah raia wa Ghana amejiunga na Simba Sc kwa uhamisho wa kudumu na kwa makubaliano maalumu.
“Uongozi wa Singida BS unawataarifu mashabiki, wapenzi na wadau wote wa soka kuwa umeridhia Simba SC kumsajili mchezaji wetu tegemeo Jonathan Sowah kwa uhamisho wa kudumu kwa makubaliano maalumu."

Aidha,taarifa hiyo imebainisha kuwa, makubaliano hayo yamefikiwa baina ya Mlezi wa Singida Black Stars na Rais wa Heshima wa Simba SC na Uongozi wa vilabu hivyo.

“Tunamtakia Jonathan Sowah kila la heri katika changamoto mpya na tunamshukuru kwa kuitumikia vyema klabu yetu katika kipindi chote alichokuwa nasi,”imeeleza taarifa ya Singida Black Stars.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news