DAR-Wachezaji watatu kutoka Azam FC Academy wameondoka nchini Jumamosi ya Julai 26,2025 kuelekea kwenye klabu ya AIK ya Sweden, kwa ajili ya mafunzo maalum ya muda wa miezi miwili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Azam FC,vijana walioondoka ni mlinzi wa kushoto Ismail Omary, viungo washambuliaji Mohammed Shillah na Adinan Rashid."Hii ni awamu ya pili kwa vijana hawa kwenda nchini humo, ambapo kwa mara ya kwanza walienda Januari 8, 2025, na kukaa huko siku 40.
"Huu ni mwendelezo wa ushirikiano kati yetu na klabu hiyo kongwe nchini Sweden, tuliyoingia nayo mkataba wa miaka mitano Septemba, 2024."