WAJUMBE wa Bodi ya Uongozi wa Wanajeshi Wastaafu (2024) SACCOS LTD na wadau wa maendeleo wamekutana kwa lengo la kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo ya kutafuta ufumbuzi wa namna ya kusaidia Wanachama wa SACCOS ambao ni Wanajeshi wastaafu kuanzisha miradi ya uzalishaji mali.


Miradi hiyo inaweza kuanzishwa kwa kuanza na fursa zilizopo ndani ya mali asili ikiwemo aridhi,misitu,ufugaji nyuki ,samaki pamoja na fursa zingine za kimaendeleo zitakazoibuliwa katika mkutano huo wa bodi na wadau hao zote zikilenga kuinua,kuboresha, kustawisha maisha ya wanajeshi wastaafu kiuchumi na kijamii.
Akizungumza Juni 30,2025 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano huo maalum ambao pia uliwezesha washiriki kupokea taarifa ya robo mwaka, mgeni rasmi Meja Jenerali mstaafu Sharif Shehe Othman amesema kuwa,mkutano huo unaenda kutengeza historia mpya ndani ya SACCOS ya Wanajeshi wastaatu chini ya Sheria ya vyama vya Ushirika.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo