Mageuzi makubwa ya sekta ya afya yamechochea mabadiliko ya maisha kwa maelfu ya wananchi wa Kagera baada ya hospitali, vituo vya afya na zahanati kusogezwa karibu na wananchi kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari Julai 1,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025 .
Mhe.Mwassa amesema,kati ya mwaka 2020 hadi Aprili 2025, Mkoa umefanikiwa kuongeza hospitali kutoka tatu hadi 11, vituo vya afya kutoka 29 hadi 42 na zahanati kutoka 217 hadi 283, hatua ambayo imepunguza umbali wa wananchi kufuata huduma na kuokoa maisha kwa wakati.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo