TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kwa mara ya kwanza wafungwa na mahabusu watapiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC, Ramadhani Kailima alisema hao Dodoma wakati akiwasilisha mada ya maandilizi ya uchaguzi na ushiriki wa vyama vya siasa kwenye mkutano wa kitaifa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).







Kailima alisema katika uchaguzi wa mwaka huu wafungwa na mahabusu watapiga kura ya urais pekee na maeneo hayo hakutakuwa na mawakala wa vyama vya siasa kutokana na usalama.
Aidha, alisema vyama vya siasa vinapaswa kuwasilisha tume majina ya wagombea wabunge na madiwani kabla au ifikapo Septemba 28, mwaka huu “Kwa upande wa majina ya wabunge na madiwani wa viti maalumu, yanatakiwa kupelekwa mwezi mmoja kabla ya uchaguzi mkuu,” alisema Kailima.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo









