TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) imeanzisha Kampasi mpya ya TIA mkoani Tanga, ambayo inalenga kuhudumia wanafunzi kutoka Kanda ya Kaskazini.
Kampasi hiyo inatajwa kuwa chachu ya kuongeza udahili wa wanafunzi kutokana na ongezeko la wahitimu katika maeneo hayo.
Akizungumza katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. William Palangyo, ameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza wigo wa elimu na kukidhi mahitaji ya soko la ajira linalobadilika kwa kasi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo