Magazeti leo Julai 6,2025

DAR-Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imewahakikishia Watanzania na wawekezaji kuwa masoko ya mitaji na dhamana nchini ni salama, hivyo wanapaswa kuyatumia kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Afisa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa CMSA, Stella Anastazi, amesema Mamlaka hiyo imeweka mazingira bora ya usimamizi ili kulinda mitaji ya wawekezaji na kuhakikisha masoko hayo yanatimiza lengo lake la msingi.





Ameongeza kuwa masoko hayo yalianzishwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuwekeza kupitia hisa za kampuni na bidhaa nyingine za masoko ya mitaji, hivyo CMSA itaendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa vyuo na kada mbalimbali ili kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika masoko hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news