DAR-Wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la BoT katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya Benki Kuu na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi kupitia mifumo rasmi ya kifedha.