MBEYA-Uongozi wa Mbeya City FC umetangaza kuachana na wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mikataba yao ya kuitumikia klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Mbeya City FC, wachezaji walioachwa ni Kilaza Mazoea, Pius Joseph, Jeremiah Thomas na Fred Mlelwa.
Wachezaji wengine walioachwa na Mbeya City FC ni Mudathir Abdallah, Andrew Kihumbi, Feisal Mganga, Medson Mwakatundu na Chesco Mwasimba.
"Uongozi wa klabu ya Mbeya City Fc unatangaza kuachana na wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mikataba yao ya kuitumikia klabu yetu , tunawatakia kila lakheri katika maisha mengine nje ya Mbeya City Fc."

