Marcio Maximo kocha mpya wa KMC FC

DAR-Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania,Marcio Maximo (63) ametambulishwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya KMC FC akichukua mikoba ya Kally Ongala aliyetupiwa virago mwezi Mei kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo.
Maximo raia huyo wa Brazil ambaye pia amewahi kuinoa Young Africans SC anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

Ujio huo wa Maximo ni jitihada za KMC FC za kujiimarisha na msimu mpya 2025/2026 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Katika utambulisho wake uliofanyika leo Julai 28, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano Manispaa ya Kinondoni, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Timu ya KMC FC,Mhe. Songoro Mnyonge amesema kuwa, kabla ya kufikia makubaliano ya kumsainisha Maximo mkataba wa mwaka mmoja kulikuwa na mazungumzo ya kina ya dira ya timu hiyo tangu akiwa kwao Brazil.

Maximo ambaye ameambatana na kocha wa viungo Bw. Wilson Toledo amesema kuwa, kabla ya kuamua kuja Tanzania alikuwa na ofa nyingi.

Amesema,ameamua kuichagua KMC FC,kwani alishawahi kuwa Tanzania kwa nyakati tofauti akiwa kocha wa timu ya Taifa Stars na Yanga SC hivyo anajisikia kuwa nyumbani akiwa Tanzania.

Maximo amesema kuwa, malengo ya KMC FC yamempa nafasi ya kuichagua kutokana na kasi ya ukuaji wa haraka wa soka la Tanzania ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news