LINDI-Mbunge wa Kilwa Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Francis Kumba Ndulane ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata ajali iliyosababisha avunjike mguu wakati wa shughuli ya usaili wa wanachama waliotangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali kupitia chama hicho.
Ajali hiyo ilitokea Julai 5, 2025 baada ya Mbunge huyo kutumbukia kwenye shimo la gereji lililopo katika karakana ya Chuo cha Maendeleo Kilwa Masoko, ambako usaili wa wagombea ubunge na udiwani ulikuwa ukiendelea.
Akizungumza Jumamosi Julai 19, 2025 kwa njia ya simu kuhusu maendeleo yake, Mbunge huyo amesema,anaendelea vizuri na amesharuhusiwa kutoka hospitali.
“Niliruhusiwa kutoka hospitali tangu Julai 15, 2025 na ninashukuru Mungu ninaendelea vizuri kwani kwa sasa kinachoendelea ni kufanya mazoezi na kusafishwa kidonda ambapo madaktari waliniruhusu nifanye hivyo katika hospitali ya karibu na nyumbani,” amesema.
Ndulane ameongeza kuwa kwa hali aliyonayo kwa sasa hata kama itatokea leo wakamtangaza kuwa ni miongoni mwa wagombea watatu waliopitishwa anao uwezo wa kwenda jimboni kutetea nafasi yake.
.jpeg)