DAR-Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Bi. Omolo ameshuhudia jinsi wataalamu wa Benki Kuu ya Tanzania wanavyotoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali, yakiwemo uwekezaji katika dhamana za serikali za muda mfupi na mrefu, mchakato wa ulipaji wa gawio kwa wawekezaji, pamoja na fursa za masomo zinazotolewa na Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania.
Amesisitiza umuhimu wa elimu kwa umma kuhusu masuala ya kifedha, ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa taifa.




