Peodoh Pacome Zouzoua ndiye mchezaji bora Ligi Kuu ya NBC mwezi Juni

DAR-Kiungo wa Yanga SC, Peodoh Pacome Zouzoua amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025, akiwashinda Clatous Chama wa Yanga na Kibu Denis wa Simba, alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Pacome ambaye ni raia wa Ivory Coast alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu ambayo Yanga ilicheza mwezi huo ambapo alifunga mabao matatu na kuhusika na bao moja kwa dakika 242 alizocheza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news