Rais Dkt.Mwinyi ashiriki dua ya kumuombea marehemu Salim Turky

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Marehemu Salim Turky.
Dua hiyo imefanyika leo Julai 20, 2025 nyumbani kwa marehemu Turky Mpendae, Wilaya ya Mjini,Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akitoa salamu zake Rais Dkt.Mwinyi, ametoa wito kwa watoto wema kuendelea kuwaombea dua wazee wao waliotangulia mbele ya haki na kuwahimiza kuendelea na mwenendo mzuri.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa amani iliodumu kwa miaka mitano inapaswa kudumishwa kwani kumekuwa na faida kubwa pamoja na amani na utulivu wa nchi kwani bila ya amani hakuna maendeleo yatakayopatikana.
Marehemu Salim Turky ametimiza Miaka 4 tangu alipotangulia mbele ya haki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news