Rais Dkt.Samia atoa shilingi bilioni 3.2 ujenzi wa shule mbili wilayani Rombo

KILIMANJARO-Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za sekondari wilayani Rombo katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Fedha hizi zimegawanyika katika shule mbili ambazo ni shule ya amali Rombo ambayo imepokea shilingi bilioni 1.6 pamoja na bilioni 1.6 zilipokewa katika Shule ya Sekondari Holili ambayo ndiyo shule mama ambapo Shule ya Kata ya Prof.Adolf Mkenda imejengwa katika Tarafa ya Mengwe katika Kata ya Holili ndani ya Kijiji cha Holili Vijijini.
Katika fedha za awamu ya kwanza ujenzi umekamilika na majengo yameanza kufanya kazi ambayo ni Madarasa 8 na ofisi 1, Jengo la utawala 1, Maabara 3 za (Fizikia, Kemia na Baiolojia), Maktaba 1, Chumba cha TEHAMA kimoja, Kichomea taka, Vyoo matundu 8 na Tanki la maji.

Katika upande wa Fedha za awamu ya pili majengo yanayoendelea na hatua za umaliziaji ni Mabweni 2, Nyumba ya mwalimu (2 in 1), Madarasa 4 na Vyoo matundu 8.
Wakati huo huo Serikali inayoongozwa na Rais Samia imetoa kiasi cha Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya na ya kisasa ya Amali (Rombo Technical Sec School) ambayo inajengwa katika Tarafa ya Mashati, Kata ya Marangu Kitowo katika kijiji cha Kitowo.

Kwa sasa ujenzi upo katika hatua za mwisho za umaliziaji kwa Madarasa 8 na ofisi 1, Jengo la utawala 1, Maabara 3 za (Fizikia, Kemia na Bilojia), Nyumba ya Mtumishi (single) 1, Maktaba 1, Chumba cha TEHAMA kimoja, Vyoo matundu 8, Kichomea taka, Tanki la maji la ardhini linatumika kuhifadhia maji kwa kazi ya ujenzi, Jengo la Karakana ya magari, Mbweni manne (4) yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 kila moja na Bwalo.
Jimbo la Rombo mkoani Kilimanjaro linaongozwa na Mheshimiwa Prof.Adolf Mkenda (Mb) ambaye ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news