Tanzania na Misri kupanua wigo wa ushirikiano

MALABO-Pembezoni mwa Mkutano wa 47 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika na Mkutano wa Saba wa Umoja wa Afrika wa Uratibu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri mwenza wa Mambo ya Nje, Uhamiaji, na Wamisri waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Dkt. Badr Abdelatty ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.
Viongozi hao wamejadili mbinu za kuimarisha na kukuza ushirikiano wa Tanzania na Misri pamoja na kuainisha maeneo mbalimbali ya kimkakati ili kuchagiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ikiwemo kukuza biashara kati ya Tanzania na utunzaji wa mazingira katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na ushirikiano katika sekta ya anga.
Aidha, wamejadili pia kuongeza ushirikiano katika biashara na kuwepo kwa ubadilishanaji ujuzi kwa wataalamu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya utalii wa mikutano na senta ya afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news