Rais Dkt.Samia azindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amezindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 huku akielezea furaha yake kwa kuona kwamba ujumuishi wa mchakato wa kuandaa hiyo umeendelea hadi katika uchapishaji wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha nakala za vitabu vya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 mara baada ya uzinduzi katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Katika uzinduzi wa dira hiyo leo Julai 17, 2025 jijini Dodoma, zimegawiwa nakala za Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa 2025 ambazo zimeandikwa kwa mfumo wa nukta nundu ili wale wenye changamoto za uoni hafifu waweze kuzisoma.

Rais Samia ametoa shukrani kwa wananchi wote ambao walijitokeza na kushiriki kutoa maoni katika mchakato wa kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, akisema kwamba ushiriki wao umeleta umiliki wa kitaifa kwenye dira hiyo.

Aidha, Rais Samia ameeleza kwamba mchakato wa uandaaji wa dira hiyo umehusisha watu wengi, na amewashukuru viongozi wastaafu wakiongozwa na Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, kwa kushiriki katika mchakato huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe mara baada ya kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe mara baada ya kuzindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya heshima na shukrani kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Profesa Kitila Alexander Mkumbo kwenye hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Wageni na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye kwenye hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kwenye hafla ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news