Serikali yajenga shule ya kisasa ya wasichana na ya amali mkoani Mwanza

MWANZA-Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imekamilisha ujenzi wa shule ya kisasa ya wasichana Mwanza ambayo imejengwa katika Wilaya ya Magu.
Shule hiyo imejengwa kupitia Mradi wa kuboresha Ubora wa Elimu Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.1 huku ikiwa na miundombinu toshelevu.

Miundombinu iliyojengwa ni pamoja na maabara nne za (Kemia, Fizikia, Baiolojia na Jografia), vyumba 22 vya madarasa na ofisi 6, Vyoo matundu 23, mabweni 9, nyumba 5 za walimu, Jengo la utawala, Bwalo, Jengo 1 la TEHAMA, Mashimo ya maji taka pamoja na fensi.
Pia,Serikali kupitia mradi huo wa SEQUIP imetoa jumla ya Shilingi Bilioni 1.6 na tayari ipo katika hatua za ukamilishaji wa ujenzi wa shule mpya ya Amali katika Kijiji cha Mhungwe kilichopo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ujenzi wa shule hiyo mpya unahusisha ujenzi wa Madarasa 8 na ofisi 2, Maktaba, Jengo la Utawala, Maabara 2 za Kemia na Baiolojia, Jengo la TEHAMA, Mabweni 4, Bwalo la chakula, Karakana 2 za ufundi Umeme na Uashi, Nyumba ya mwalimu, na Matundu 8 ya vyoo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news