Ujumbe kutoka PPAA wawasili Kosovo kwa ziara ya kikazi

PRISHTINA-Ujumbe kutoka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Awadh Bawazir umewasili Jijini Prishtina nchini Kosovo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 14 – 18 Julai, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kosovo Bw. Ilir Muçaj akizungumza na ujumbe kutoka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) unaoongozwa na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Awadh Bawazir baada ya kuwasili Jijini Prishtina nchini Kosovo kwa ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia tarehe 14 hadi 18 Julai, 2025.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani ameambatana na Wajumbe wa Mamlaka ya Rufani, Kamishna wa Idara ya Sera za Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga, Mkurugenzi wa Mipango Wizara ya Fedha, Bw. Moses Dulle pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya PPAA.
Mwenyekiti wa Ujumbe huo, Jaji Mstaafu Mhe. Awadh Bawazir ameeleza lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kupata uzoefu wa taasisi zinazosimamia ununuzi wa umma na mnyororo wa ununuzi wa umma hususan katika masuala ya ununuzi wa umma, uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroni nchini Kosovo.
Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Prishtina, ujumbe wa Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma ulipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kosovo, Bw. Ilir Muçaj.
Ujumbe huo ukiwa nchini Kosovo unategemea kutembelea Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PRD), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRC), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAO), pamoja na Idara ya Uratibu wa Ukaguzi wa Ndani (CHDIA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news