Serikali yamfikia mtoto aliyeonesha kipaji ujenzi wa barabara na madaraja

DODOMA-Kufuatia video fupi iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikimuonesha mtoto, Riziwani Martin Asheri mwenye umri wa miaka 13, mkazi wa Kibaigwa mkoani Dodoma ambaye ana kipaji cha kujenga barabara na madaraja, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega alituma maafisa kutoka wizarani kumtembelea mtoto huyo ili kupata ukweli wa taarifa hiyo.
Maafisa hao walipata fursa ya kuzungumza mengi na mtoto huyo, mama yake, mjomba wake na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Karume ambapo walieleza mambo kadhaa kuhusu historia ya maisha ya mtoto huyo kwa ujumla na elimu yake.
Pia,walielezwa kuhusu ndoto za mtoto huyo ambaye anatamani akiwa mkubwa aje kuwa mhandisi mkubwa nchini atakayeleta maendeleo kupitia sekta ya Ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news