DAR-Klabu ya Simba SC imethibitisha kuachana na kiungo Fabrice Luamba Ngoma raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia baada ya kumalizika kwa mkataba wake,hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2025/2026.
Ngoma mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na kikosi cha Simba Sc mnamo Julai,mwaka 2023 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Hilal ya Sudan.
