Soko Kuu jipya la Kariakoo mbioni kufunguliwa

DAR-Ujenzi wa Soko Kuu jipya la Kariakoo jijini Dar es Salaam umefikia takribani asilimia 99 na uko katika hatua za mwisho kabla ya kuzinduliwa rasmi.
Mradi huu unatekelezwa na Estim Construction Ltd kwa usimamizi wa kitaalamu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na umekamilishwa kwa viwango vya juu vya ubora.

Mradi unahusisha ujenzi wa jengo jipya lenye ghorofa nne juu ya ardhi na ghorofa mbili za chini (basement) pamoja na ukarabati wa soko la zamani, kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 28.

Mara utakapokamilika, soko jipya litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 2,300, sawa na ongezeko la zaidi ya wafanyabiashara 600 kutoka 1,662 waliokuwepo awali. Pia litakuwa na miundombinu ya kisasa, maeneo ya kuhifadhia bidhaa, mifumo ya zimamoto, na nafasi za upakiaji na upakuaji mizigo.
Soko Kuu la Kariakoo liliungua Julai 10, 2021, na Serikali ilianzisha mchakato wa kujenga upya ili kuhakikisha usalama na ufanisi wa biashara katika eneo hilo muhimu. Ujenzi unatarajiwa kukamilika kikamilifu na kuzinduliwa hivi karibuni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here