Wizara ya Eimu na Diaspora kushirikiana utekelezaji wa Samia Scholarship Extended

DAR-Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ameongoza kikao kati ya Wizara na Watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) walio katika fani za Sayansi ya Data, Akili Unde na Sayansi shirikishi.
Kikao hicho kimefanyika Julai 20, 2025 kwa njia ya Zoom na kushirikisha Dispora kutoka nchi mbalimbali kikilenga kuzungumzia ushirikiano katika utekekezaji wa programu ya Samia Scholarship Extended DS/SI+.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki hao wamepongeza hatua ya Wizara kuanzisha programu hiyo na kwamba watashirikiana na Serikali katika kufanikisha ili kuongeza Idadi ya Watanzania Wataalamu katika Fani hizo kwa kusaidia kutoa ushauri wa kitaalamu, kutafuta fursa na masomo kwa watakaokidhi vigezo na hata kutoa mafunzo.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo, Kamati maalum inayoratibu programu hiyo inayoongozwa na Prof Makenya Maboko, pamoja na viongozi wengine kutoka Wizarani, NM-AIST na COSTECH.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news