CUF yafukuza wanachama saba

DAR-Chama cha Wananchi (CUF) kimewafukuza wanachama wake saba kwa utovu wa nidhamu na kukiuka masharti ya katiba ya chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 8, 2025 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema, wanachama hao wameongoza vurugu na kupinga kusaini mahudhurio.

Waliofukuzwa ni Dauda Hassan Kasigwa, Yasin Mrotwa, Abdallah Dadi Ubwa, Faki Suleiman Mohamed, Rashid Ali Hamad, Mohammed Nassor Hamad na Yusuf Ali Mussa.

Pia, katika mkutano huo ametaja majina ya waliopendekezwa na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho Agosti 6,2025 ambao watapigiwa kura katika mkutano wa Agosti 9,2025 kuwakilisha chama katika nafasi za urais.

Kwa upande wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Gombo Sambandito Gombo na Nkunyuntila Siwale.

Aidha,kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliopendekezwa kugombea nafasi ya Urais ni Mhandisi Mohamed Habib Mnyaa, Mhandisi Hamad Masoud Hamad na Dkt. Mohamed Habib Mikidadi.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum watapiga kura kwa ajili ya kumpata Mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CUF katika kampeni za Uchaguzi Mkuu Oktoba,mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news