DAR-Rais wa klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said amewatangazia wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa klabu hiyo kuwa kutakuwa na Mkutano Mkuu wa kawaida utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 07/09/2025 kuanzia saa nne kamili asubuhi.
Mkutano huo utakaofanyika kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2021 utafanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) uliopo posta jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Agosti 8, 2025 iliyotolewa na Rais Eng. Hersi imeorodhesha ajenda za Mkutano huo ambazo ni pamoja na;
1. Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa wajumbe wanaohudhuria mkutano.
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.
5. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji.
8. Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia, pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya Klabu.
9. Kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofata.
10. Kufunga Mkutano
Tags
Engineer Hersi Said
Habari
Mhandisi Hersi Said
Michezo
Yanga SC
Young Africans SC
Young Africans Sports Club

