Dkt.Biteko akoleza kasi matumizi ya nishati safi nchini

DODOMA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewataka watumishi katika Wizara ya Nishati na taasisi zilizochini ya wizara hiyo kuwa mfano katika matumizi ya Nishati Safi ya kupikia ili kuitekeleza kwa vitendo ajenda iliyoasisiswa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama kwa afya.
Dkt.Biteko ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22,2025 jijini Dodoma wakati akigawa majiko yanayotumia umeme kidogo kwa watumishi wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambapo amewataka Watumishi hao wawe mabalozi katika kutekeleza ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia.

"Leo tunagawa majiko haya kwa kuwa nyinyi ndiyo wenye dhamana kuu ya kutekeleza Ajenda ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, hivyo wajibu wenu ni mabalozi wazuri kwa watu wanaowazunguka ili nao wahamasike kutumia nishati hii safi,"amesema Dkt.Biteko.

Amesema,kufuatia mwamko mkubwa unaoendelea sasa kwa wananchi kufahamu faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia, kiwango cha watumiaji kimepanda kutoka asilimia sita na kufikia asilimia 20.3 huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 80 ifikapo 2034.
Dkt. Biteko amebainisha kuwa, idadi ya watu wanaoendelea kutumia nishati isiyo safi na salama ya kupikia bado ni kubwa duniani, barani Afrika na hapa Tanzania hivyo ni jukumu la watumishi wote wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kuhakikisha watanzania wanapata elimu sahihi ili waweze kubadilika na kufikia lengo lililokusudiwa.

Akigawa majiko 220 kwa watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt. Biteko amepongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan katika maeneo ya vijijini ambapo kumeonekana kuwa bado changamoto ya kufikiwa na Nishati Safi ya Kupikia.
Pia, ameipongeza REA kwa kuhakikisha Vijiji vyote 12,318 nchini vinafikiwa na umeme.Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amemhakikisha Dkt. Biteko kuwa atakahikisha agizo alilolitoa linatekezwa na Taasisi zote anazozisimamia.
Amesema atahakikisha kwamba Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia yanafikia malengo yaliyokusudiwa.

Amewasisitiza watumishi kutumia Majiko hayo waliyopewa na si kuyahifadhi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news